Nahodha wa Chelsea FC, Reece James amesaini mkataba mpya wa miaka sita utakaoendelea kumbakisha katika klabu hiyo hadi majira ya joto ya mwaka 2032. Hatua hiyo imekuja wakati mkataba wake wa awali ulikuwa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028, huku klabu ikiamua kumfunga kwa muda mrefu zaidi ili kuondoa uvumi wa uhamisho kuelekea dirisha la usajili la majira ya joto.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 26 amekuwa sehemu ya Chelsea tangu akiwa na umri wa miaka sita, na amesema ana furaha kubwa kuongeza muda wa kuitumikia klabu hiyo ya London Magharibi. James amesema kusaini mkataba mpya ni jambo linalompa faraja na furaha kubwa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Nina furaha sana kuongeza mkataba wangu. Chelsea ina maana kubwa sana kwangu. Nimekuwa nikisema kila mara kwamba nataka kutumia miaka yangu bora hapa, na ninaamini tuna kila kitu kinachohitajika kujenga mafanikio zaidi,” amesema James kupitia tovuti rasmi ya klabu hiyo.
James, ambaye alicheza mechi yake ya kwanza mwaka 2019, hadi sasa ameichezea Chelsea michezo 225 na aliteuliwa kuwa nahodha wa timu hiyo mwaka 2023. Licha ya kukumbwa na majeraha kadhaa katika misimu ya hivi karibuni, bado anaendelea kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi kinachonolewa na kocha Liam Rosenior.
Chini ya uongozi huo, Chelsea ilifanikiwa kutwaa mataji ya UEFA Europa Conference League pamoja na FIFA Club World Cup mwaka uliopita. Wakurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Paul Winstanley na Laurence Stewart wamesema ni fahari kubwa kwa klabu kuona James akiendelea kubaki, wakimtaja kama kiongozi muhimu ndani na nje ya uwanja.

