Kocha mkuu wa AC Milan Stefano Pioli amesisitiza kuwa AC Milan hawakuvurugwa na mechi yao inayokuja ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Salzburg wakati walipopoteza wakiwa ugenini dhidi ya Torino kwa mabao 2-1.

Mabao ya Torino yalifungwa katika kipindi cha kwanza cha mcheza, ambapo katika dakika ya 35 Koffi Djidji aliiandikia bao la kwanza timu yake na dakika mbili baadae Miranchuk akapachika bao la pili na baadae Milan kupata bado la kufuatia machozi dakika ya 67.
Pioli na vijana wake wakamaliza mchezo huo kwa kupoteza huku ikiwa ni mchezo wa pili kwao kupoteza kwenye Serie A msimu huu na sasa wameachwa pointi 6 na vinara wa ligi hiyo Napoli.
Milan itamkaribisha Salzburg hapo kesho kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa ambapo atahitaji pointi moja tu ili aweze kuungana na Chelsea ambaye ameshafuzu katika hatua inayofuata katika kundi E, huku Pioli akisema kuwa ana uhakika kuwa wa kufanya vyema.

Kocha huyo hakuishia hapo aliongeza kwa kusema kuwa ili wajiandae vyema kwenye ligi ya Mabingwa walilazimika kufanya vyema kwenye mchezo wa jana lakini hawakufikiria juu ya hilo hata kidogo.
Pioli aliiambia DAZN kuwa haukuwa usiku mzuri kwao na hilo ni dhahiri kabisa baada ya kushindwa kupata matokeo. “Nilijaribu kubadili mashambulizi, lakini tulihitaji kuchukua nafasi mapema kidogo, kucheza kidogo, na hatukufanikiwa kurejesha mabao yote”.


