Ligi kuu ya NBC kuendelea hii leo kwa michezo miwili ambapo mchezo mojawapo wa kuvutia ni kati ya Azam FC dhidi ya KMC majira ya saa 1:00 usiku.

 

Azam FC mechi iliyopita ametoka kupata sare dhidi ya mnyama huku KMC yeye akipoteza dhidi ya kinara wa ligi Yanga kwa bao 1-0.


Wanalamba lamba amabo wapo chini ya Kally Ongala wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza michezo yao 23, ameshinda mechi zake 13, sare tano, na kupoteza mara tano.

Wakati kwa upande wa KMC, wao wapo nafasi ya 12, wakishinda michezo mitano, sare nane na wamepoteza michezo 10 hadi sasa. Wana pointi zao 23 baada ya kupoteza michezo yao mitatu mfululizo.

Mechi ya kwanza kukutana kati yao KMC aliondoka na ushindi. Je leo hii Matajiri wa Chamazi watavuna pointi ngapi au watanyolewa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa