Ihefu Yaicharaza Dodoma Jiji na Kuchukua Pointi 3

Timu ya Ihefu FC imejikusania pointi tatu hapo jana baada ya kuicharaza Dodoma Jiji akiwa kwao kwenye mchezo wa Ligi kuu ya NBC hapo jana kwa mabao 2-1.

 

Ihefu Yaicharaza Dodoma Jiji na Kuchukua Pointi 3

Mchezo huo ulipigwa majira ya saa 1:00 usiku ambapo mwenyeji Dodoma alisindwa kufurukuta mbele ya vijana hawa kutoka Mbeya ambapo mabao ya ushindi yalitupiwa kimyani na Nelson Okwa na Yacouba Songne.

Huku bao la kufutia machozi kwa upande wa Dodoma lilifungwa na Malima na kuwafanya waendelee kushika nafasi ya 11 baada ya kupoteza mechi ya pili mfululizo kwenye ligi kuu hadi sasa.

Bado una nafasi ya kucheza kasino ya mtandaoni ukiwa na Meridianbet kama vile Poker, Roulette, Aviator. Ingia na ucheze sasa.

Baada ya ushindi huo timu ya Ihefu imepanda hadi nafasi ya 7 baada ya kujikusanyia alama 30 kwenye msimamo.

Ihefu Yaicharaza Dodoma Jiji na Kuchukua Pointi 3

Dodoma jiji bado wana kibarua kikubwa cha kufanya chini ya kocha mkuu Melis Medo ambaye anahitajika kufanya juhudi ili timu hiyo isishuke daraja.

Acha ujumbe