Dodoma Jiji Uso kwa Uso Dhidi ya Ihefu

Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara kuendelea hii leo kwa michezo miwili ambapo moja ya mchezo wa kuvutia ni ule utakaowakutanisha kati ya Dodoma Jiji dhidi ya Ihefu majira ya 1:00 usiku.

 

Dodoma Jiji Uso kwa Uso Dhidi ya Ihefu

Dodoma Jiji wapo nafasi ya 11, baada ya kucheza michezo yao 23, wakiwa wameshinda michezo sana wakaenda sare michezo mitatu huku wakipoteza mara 13 hadi sasa, na mchezo wa mwisho wamepoteza.

Wakati kwa upande wa Ihefu wao wapo nafasi ya 9 kwenye msimamo, wakishinda mechi zao nane, sare tatu na kupoteza michezo yao 12, pointi 27 kibindoni hadi wakati huu, na mechi ya mwisho katoa sare.

Dodoma Jiji Uso kwa Uso Dhidi ya Ihefu

Tofauti ya pointi kati yao ni nne pekee, huku mechi tatu za mwisho kukutana Dodoma maeshinda moja huku Ihefu wao wakishinda mbili.

 

 

Acha ujumbe