Azam FC kuinunua Baobab Queens

TIMU ya Azam FC inasemekana kuwa wameichukuwa timu ya Baobab Queens kwa mwaka mmoja ili kutimiza agizo la Shirikisho la Soka Africa (CAF) la kutaka timu zote zitazoshiriki mashindano yao msimu ujao lazima zimiliki au kuwa mshiriki wa timu za wanawake.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Baobab kimesema kuwa mchakato wa Azam FC kuichukua timu hiyo ulianza tangu mwaka jana ila ukakwama na sasa wamerejea tena na wapo tayari kufanya hivyo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Azam FC Thabity Zakaria (Zaka) alipotafutwa ili kupata ukweli wa taarifa hizo alisema kwa upande wake hana uthibitisho wa hizo taarifa ingawa anafahamu kulikuwa na kitu kama hicho.

“Sina taarifa rasmi juu ya hicho unachosema, ingawa nafahamu kuna mchakato wa namna hiyo ulikuwepo chini ya viongozi wa Azam FC,” alisema.

Azam FC ambao tayari imeshapata tiketi ya kucheza Kombe La Shirikisho Afrika inalazimika kutimiza takwa la CAF la kuwa na timu ya wanawake au kujihusisha na mpira wa wanawake ili kupata kibali cha kushiriki mashindano hayo msimu ujao

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.