BALEKE KIBOKO YA MTIBWA YUKO FITI

MKALI wa Uwanja wa Manungu kwa msimu wa 2022/23 Jean Baleke yupo kamili kuikabili timu hiyo akiwa na kazi ya kuvunja rekodi yake aliyoandika kwenye uwanja huo.

Ni Feisal Salum huyu aliyekuwa ndani ya Yanga msimu wa 2022/23 na sasa ndani ya Azam FC ameandika rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kufunga hat trick kwenye ligi.BALEKEIkumbukwe kwamba msimu uliopita Feisal alipokuwa Yanga hakufunga hat trick hivyo ameanza na rekodi mpya ndani ya uzi mpya.

Machi 13 2023 Baleke aliandika rekodi ya kufunga hat trick kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Manungu.

Katika mchezo huo Baleke alitupia kambani mabao hayo yote kipindi cha kwanza ilikuwa dakika ya 3, 6 na 33 akiwa ndani ya 18.

Kikosi cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira leo kinatarajiwa kumenyana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa wachezaji wote wa Simba wapo tayari kwa ajili ya kupambana kwenye mashindano ambayo wanashiriki.BALEKE“Wachezaji wote wapo tayari kuwapa burudani mashabiki wa Simba kikubwa ni wao kujitokeza uwanjani kuishangilia timu yao,” .

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo kambini Morogoro ni pamoja na Jean Baleke, Fabrice Ngoma pia kipa mpya Ayoub Lakred naye yupo ndani ya kikosi hicho.

Acha ujumbe