Liverpool na Man United Vitani kwa Kiungo Bayern

Klabu ya Liverpool na Manchester United zitaingia vitani katika kumuwania kiungo wa klabu ya Bayern Munich raia wa kimataifa wa Uholanzi Ryan Gravenberch.

Kiungo Ryan Gravenberch amekua hapati nafasi mara kwa mara ndani ya klabu ya Bayern Munich ambapo klabu ya Manchester United na Liverpool wanaona kama itakua nafasi nzuri ya kumshawishi kiungo huyo wa zamani wa klabu ya Ajax.liverpoolKlabu ya Bayern Munich wenyewe wanaelezwa wamesimama katika msimamo wao kua kiungo huyo hauzwi licha ya kuonekana hapati nafasi klabuni hapo, Lakini vyanzo vinaeleza kua Gravenberch anaweza kukubali kuondoka klabuni hapo na kwenda klabu ambayo atakua anapata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Man United mpaka sasa wako sokoni kutafuta kiungo na vijogoo wa Anfield nao wako mawindoni kwajili ya kutafuta kiungo mwingine baada ya kumsajili kiungo Endo jana kutoka klabu ya Stuttgart kutoka nchini Ujerumani.liverpoolKlabu ya Liverpool na Manchester United watahitaji kufanya kazi ya ziad kuishawishi klabu ya Bayer Munich kumuachia kiungo huyo,Lakini ambaye atafanikiwa kwenye vita hiyo baina ya vilabu hivo viwili ni ambae ataweka ofa nono mezani.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.