Mudryk Aomba Uvumilivu Chelsea

Winga wa klabu ya Chelsea raia wa kimataifa wa Ukraine Mykhailo Mudryk ameomba uvumilivu ndani ya klabu hiyo kutokana na kiwango chake ambacho anakionesha kwasasa.

Mudryk ambaye amekua akinyooshewa kidole na mashabiki wa klabu hiyo tangu alipojiunga na timu hiyo mwezi Januari mwaka huu,Kutokana na kutokuonesha ubora mkubwa kama ambao alikua anauonesha ndani ya klabu ya Shakhtar Donetsk.mudrykWinga huyo amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuangalia ubora wa Vinicius Jr ambao alikua nao katika msimu wake wa kwanza ndani ya Real Madrid ukilinganisha na sasa, Hii akimaanisha wachezaji wanahitaji muda ili kuonesha ubora wao.

Kutokana na kauli ya mshambuliaji huyo ni wazi anaamini atakua kwenye ubora mkubwa katika siku za usoni ndani ya klabu hiyo, Huku akiamini kwenye muda zaidi kama  ambavyo Real Madrid walimvumilia Vinicius Jr na sasa anawalipa kutokana na ubora wake.mudrykWinga Mudryk ni mchezaji ambaye ana ubora mkubwa na hilo amelidhihirisha ndani ya klabu yake ya Shakhtar Donetsk,Lakini pia ndani ya timu a taifa ya Ukraine kwa Chelsea mambo yamekua tofauti lakini yeye mwenyewe anaamini atafanya vizuri ni suala la muda tu.

Acha ujumbe