BEKI KINDA YANGA APATA NAMBA

KATIKA kuhakikisha safu ya ulinzi inafanya vema, Kocha Mkuu wa Yanga Muargentina amempandisha beki wa kati kinda, Shaibu Mtite.

Kinda huyo ana kibarua kigumu cha kupambania namba mbele ya Gift Fred, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Bacca.

Beki huyo yupo kambini tangu ilipoingia kambini Kijiji cha Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.yangaMtoa taarifa huyo alisema kuwa beki huyo amepandishwa na Gamondi baada ya kuvutiwa na kiwango chake ambacho amekionyesha akiwa katika kikosi cha vijana cha U20.

Aliongeza kuwa kocha wa Yanga amempa matumaini ya kucheza katika kikosi hicho katika msimu ujao, licha ushindani uliokuwepo katika timu hiyo.

“Mtite ni kati ya wachezaji tuliowasajili kwa ajili ya msimu ambaye amepandishwa katika kikosi cha wakubwa akitokea timu yetu ya vijana.

Gamondi ndiye aliyependekeza usajili wake baada ya kuvutiwa na kiwango chake.

Gamondi ni muumini mzuri wa vijana, hivyo amepanga kuwapandisha wachezaji wengine vijana katika kila msimu.

Gamondi alizungumzia kiwango cha beki na kusema kuwa ” Mtite ni kati ya wachezaji wanaochipukia ambaye ninaamini atafanya makubwa siku za usoni.

Acha ujumbe