Gamondi Awamaliza Al MERREIKH Mapema

GAMONDI

KOCHA Mkuu wa Yanga, Muargentina Miguel Gamondi amesema kuwa atatumia siku tano kuwasoma wapinzani wake Al Merreikh ya Sudan kabla ya kukutana. Unaweza kutumia sekunde chache kuwa tajiri ukibeti Meridianbet.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana hivi karibuni katika hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Yanga imefuzu hatua hiyo, baada ya kuwaondoa ASAS ya nchini Djibouti kwa ushindi wa mabao 6-1 katika mchezo wa nyumbani na ugenini. Mechi za klabu bingwa Afrika zina odds kubwa na machaguo kibao Meridianbet.

Gamondi alisema kuwa, mara baada ya mchezo wa ASAS sasa nguvu na akili zake anazielekeza mchezo ujao dhidi ya Merreikh kwa ajili ya kufanya maandalizi.

Gamondi alisema kuwa, hivi sasa atakachokifanya ni kuwasoma Merreikh kwa kutumia video katika michezo ya Ligi Kuu ya Sudan na ile ya Ligi ya Mabingwa Afrika waliyocheza msimu huu.

Unaweza kucheza sloti na kasino ya mtandaoni ya Meridianbet ikiwa tu wewe si mpenzi wa kubashiri soka.

SHINDA

Aliongeza kuwa anaamini Al Merreikh wamefanya maingizo mapya ya wachezaji, hivyo ni lazima apate video mpya za mechi zao walizozicheza msimu huu.

“Tumemaliza mechi yetu ya ASAS, hivyo sasa hivi tunahamishia maandalizi yetu ya mchezo ujao dhidi ya Al Merreikh.

“Ni lazima niwasome Al Merreikh kwa kutumia video za mwisho za mashindano walizozicheza ili kujua ubora na udhaifu wa wapinzani wetu ili tutakaporudiana tusipate ugumu,” alisema Gamondi.

Acha ujumbe