Mchezaji wa Azam FC Idd Seleman Nado ameipatia timu yake pointi tatu hapo jana baada ya kupachika bao moja ambalo liliipa ushindi timu yake mpaka dakika 90 za mchezo kumalizika.
Azam FC walikuwa wakimenyana dhidi ya KMC katika dimba la Chamazi majira ya saa 1:00 usiku huku timu hiyo ambayo ipo chini ya Kally Ongala ikijipatia ushindi mwembamba nyumbani kwao.
Baada ya kufunga bao hilo la ushindi na muhimu sana hapo jana amefikisha mabao manne kwenye ligi kuu hadi sasa.
KMC baada ya kupoteza jana amefikisha mechi nne mfululizo akifungwa huku ndani ya mechi nane, ameshinda moja sare moja na kapoteza michezo sita. Yupo nafasi ya 13 baada ya kukusanya pointi 23.
Azam FC wao wapo nafasi ya tatu baada ya ushindi wa jana wakiwa wamejikusanyia pointi 47 kwenye msimamo wa ligi huku mechi ijayo wakitarajia kumenyana dhidi ya Ihefu ugenini.