Kiungo mshambuliaji wetu, Idd Seleman ‘Nado‘, ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia kwenye viunga vya Azam Complex.
Nado amesaini mkataba huo leo Jumanne mchana mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya aendelee kusalia Azam FC hadi mwaka 2024.

Nyota huyo amekuwa na kiwango tokea msimu uliopita alipojiunga nasi akitokea Mbeya City, hadi sasa msimu huu akiwa amehusika kwenye mabao 12 ya Azam FC, akifunga mara saba na kutoa pasi za mwisho tano.

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.



dorophina
Habari njema kwa mashabiki wa azam
Angelina
Nice update
Venerose
Hongera sana IDD
Hopemwaikuka
Gud
warda
Anajitahidi sana