Nchimbi, Winner Never Quits

Nakuuliza swali ewe mwana wa Mzee Nchimbi ila usinijibu, je kama anakufa kwa asali, kwanini umpe sumu? Siku ya 15 ya Januari 1929 pale Atlanta, Georgia, Marekani alizaliwa Mkombozi wa Watu weusi, aliitwa Martin Luther King jr.

Huyu alikua mwanaharakati tishio kwa ngozi nyeupe, wala hakushika mtutu kuidai haki, ulimi wake ulikua zaidi ya AK47, Wasomi wote wa Historia hawataisahau Agosti 28 1963 ilipotoka Hotuba ya Ndoto, alisikika Martin akisema “I have a Dream” yes kwanza tukomee hapa ewe Nchimbi.

Ulimwengu wote unatambua kila kilichomo ndani yake (Ulimwengu ) kina ndoto, naamini thamani ya ndoto yako unaijua wewe Nchimbi na una uchu wa kuitimiza, ebu tumsikilize tena Martin.

Aliendelea kupanda mbegu za uzalendo kwa watu weusi huko Marekani kisha akasema “We must accept finite disappointment, but we must never lose infinite hope.” Lazima tukubali kukatishwa tamaa kabisa, lakini hatupaswi kupoteza tumaini kubwa.”

Naam!!, Hapa ndipo kwenye shina la mti huu ninaokupandia wewe Nchimbi, Kila mwenye Ndoto hukatishwa tamaa, hatuwezi kuepuka hali hii bali tunaweza kupambana nayo. Siku hizi changamoto ni Fursa, itumie fursa hii kuweka amani kwa Wananchi.

Wacha nikukumbushe masahibu ya Wesley Sneijder na Ajax yake mwaka 2002 mpaka 2007, kwa miaka mitano aliyocheza alifunga magoli 43 licha ya kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, leo hii nani hamjui Wesley.

Nchimbi
Wesley Sneijder

Eti Nchimbi, Hivi humjui Luis Nani aliyekaa miaka 9 Man United na kufunga magoli 25 tu, lakini hakauki timu ya Taifa, basi usiwaze sana swala lako la kutimiza mwaka pasi na kufunga, au umemsahau Antonio Cassano Lulu ya Italia? Straika aliyecheza miaka 18 lakini hajafikisha hata magoli ya John Bocco?

Nchimbi
Luis Nani

Usinung’unike Nchimbi, huu ndiyo wakati wako, usimtafute mchawi wala usiende baharini kuoga maji ya kutoa mikosi, mungu yupo na kila anayemuomba, mazoezi na bidii ndiyo silaha yako, kama ndoto ya Martin Luther king ilitimia, basi na yako itatimia.

Dawa ya mashabiki ni magoli yako tu, na hiyo ndiyo asali kwao, wape asali, usiwape sumu kwa kufanya maamuzi mabaya, A quitter never wins and a winner never quits. Umri bado mdogo.


JILIPE KWA NAMBA ZAKO ZA BAHATI NA KENO

Kila mtu ana namba zake za bahati, Meridianbet tunatambua namba zinaweza kukufanya milionea leo. Jilipe kwa namba zako za bahati kila baada ya dakika tano.

CHEZA HAPA

5 Komentara

    Nice update

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Asanteni kwa makala

    Jibu

    Kabsaa

    Jibu

    Hata hajui

    Jibu

Acha ujumbe