ISHU YA AZAM NA KITAYOSE IPO HIVI

KUFUATIA mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Azam FC dhidi ya Kitayosce ya Tabora kutokamilika dakika 90 uongozi wa Bodi ya Ligi Tanzania umetolea ufafanuzi suala hilo.

Ni Yanga wao walitwaa taji la ligi msimu wa 2022/23 wana kazi ya kutetea taji hilo kwa msimu mpya wa 2023/24.

Mchezo wa kwanza kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex itakuwa dhidi ya KMC.AZAMIkumbukwe kwamba Agosti 16 Uwanja wa Azam Complex mchezo huo ulichezwa lakini hazikugota dakika 90 kama ambavyo mechi za ligi nyingine huchezwa.

Wakati mchezo unasimamishwa kwa mujibu wa kanuni baada ya majadiliano Azam FC walikuwa wanaongoza kwa mabao manne huku nyota Feisal Salum akifunga hat trick ya mapema zaidi na ikiwa ni ya kwanza msimu wa 2023/24.

Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda, amebainisha kuwa Azam FC wamepewa pointi tatu na mabao (4) yaliyofungwa katika mchezo huo yanahesabiwa.

Hivyo Azam wanaongoza ligi na Feisal aliyeibuka ndani ya kikosi cha Azam FC akitokea Yanga anaongoza kwa mabao akiwa nayo matatu kibindoni licha ya mchezo kusimamishwa dakika ya (18).

Boimanda amesema kwa mujibu wa kanuni timu ikiwa na wachezaji (7) inaruhusiwa kucheza mchezo ndio maana waliruhusu mchezo uendelee licha ya kuwa Kitayosce walikuwa na wachezaji (8).AZAMAmebainisha kwa kusema kuwa, wao walipokea majina ya wachezaji (8) wanaoruhusiwa kucheza kutoka kwenye mamlaka (TFF).

Wachezaji wengine wa Kitayosce waliosajiliwa wamezuiwa kucheza mabao kwenye mchezo huo yalifungwa na Feisal Salum dakika ya tatu 09′, 13′ na bao moja ni mali ya Prince Dube dakika ya tano.

Acha ujumbe