Ligi kuu ya NBC inaendelea leo kwa michezo miwili huku mchezo wa kwanza utakuwa ni ule unaowakutanisha kati ya Singida Big Stars dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Liti huko Singida.

Mchezo huo utapigwa majira ya 10:00 jioni huku Singida wakikumbuka kupoteza mechi yao ya kwanza walipokutana huko Chamazi na leo ni zamu yao kulipiza kisasi na kusaka pointi 3 wakiwa nyumbani.
Azam wapo nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza mechi zao 20 wakiwa na pointi zao 43, baada ya kushinda mechi zao 13, sare nne na kupoteza michezo mitatu, huku Walima alizeti wao wakiwa nafasi ya nne, pointi 40.

Tofauti kati yao ni pointi tatu pekee, huku mechi 5 za mwisho Wanalamba lamba wameshinda mbili, sare mbili na wamepoteza moja. Vijana wa Pluijm wao wameshinda nne na sare moja.

