Manchester City wanakimbiza Mwizi Kimyakimya

Klabu ya Manchester City unaweza kusema ni kama wanakimbiza mwizi kimyakimya kwenye ligi kuu ya Uingereza ni baada ya kupata alama tatu muhimu dhidi ya klabu ya Wolverhampton.

Manchester City wamefanikiwa kuifunga klabu ya Wolverhampton kwa mabao matatu kwa bila na kufikisha jumla ya alama 47 wakiwa nyuma ya vinara wa ligi hiyo kwa alama 2. Klabu ya Arsenal wanaongoza ligi wakiwa na alama 47 huku City wao wakiwa na alama 45.Manchester cityMshambuliaji wa klabu hiyo Earling Braundt Haaland ndio amepeleka kilio kwa klabu ya Everton baada ya kufanikiwa kufunga mabao yote matatu katika mchezo huo na kuisaidia timu yake kushinda mchezo huo. Mshambuliaji huyo amefanikiwa kufikisha mabao 25 katika ligi hiyo baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa leo.

Klabu ya Manchester City inaonekana sasa kurejea kwenye mbio za ubingwa baada ya kufanikiw akupunguza pengo la alama kutoka alama nane mpaka alama kufikia pengo la alama mbili. Vijana wa Pep Guardiola wanaonekana kuanza kuutaka tena ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza.Manchester cityManchester City wamepata faida ya kuanza kucheza kabla ya wapinzani wao klabu ya Arsenal ambao wana kibarua kizito jioni ya leo dhidi ya klabu ya Manchester United, Ikiwa klabu ya Arsenal wataweza kushinda mchezo wao dhidi ya Man United basi watarudisha pengo la alama na kurudia kua alama tano.

Acha ujumbe