Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Earling Haaland hashikiki kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kufunga mabao matatu leo katika mchezo kati ya klabu yake na Woverhampton.

Haaland tayari amefanikiwa kufunga mabao 25 baada ya kufunga mabao matatu katika mchezo wa leo dhidi ya Wolves huku akiwa ndio kwanza ukiwa mchezo wa kwanza kwenye mzunguko wa pili kwenye ligi kuu ya Uingereza.HaalandMshambuliaji huyo mpaka sasa ameshafunga mabao 25 katika michezo19 ya ligi kuu ya Uingereza aliyocheza mpaka wakati huu, Hii inaonesha ni kwa namna gani mshambuliaji huyo ana ubora mkubwa katika suala la kuzifumania nyavu kunako ligi kuu ya Uingereza.

Earling Haaland mpaka sasa amefanikiwa kuwapiku wafungaji bora wa ligi kuu ya Uingereza msimu uliomalizika ambao walikua na magoli 23 kila mmoja ambao ni Mohamed Salah na Heung Ming Son, Lakini mshambuliaji huyo katumia michezo 19 tu kufikisha mabao 25.HaalandMshambuliaji huyo pia anafunga mabao matatu kwenye mchezo mmoja kwa mara ya nne ndani ya msimu huu kwa maana mpaka sasa Haaland ana Hattrick nne. Mshambuliaji huyo kila uchwao anavunja rekodi katika ufungaji wa mabao huku kukiwa na kila dalili ya kuvunja rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye msimu mmoja ambayo inashikiliwa na Alan Shearer na Andy Cole ambao walimaliza na mabao 34.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa