Klabu ya Manchester City leo itashuka dimbani katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Tottenham Hotspurs mchezo utakaopigwa katika dimba la Etihad.
Klabu ya Manchester City itakua kwenye mtanange mkali leo dhidi ya klabu ya Tottenham mchezo unaotarajiwa kua mgumu sana na wenye kuvutia tu, Klabu hizo zinakutana wakati ambao kila timu inahitaji alama tatu muhimu zaidi baada ya kupoteza michezo yao iliyopita.
Klabu ya Manchester City ilipoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya mahasimu zao klabu ya Manchester United hivo katika mchezo wa leo itakua inahitaji alama tatu muhimu ili kupunguza pengo la alama baina yao na vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya Arsenal.
Klabu ya Tottenham Hotspurs yenyewe imepoteza mchezo uliomalizika dhidi ya mahasimu wao pia klabu ya Arsenal ambapo walipoteza kwa mabao mawili kwa bila, Hivo mchezo wa leo dhidi ya vijana wa Guardiola utakua ni mchezo muhimu zaidi kwao kuweza kupata alama tatu.
Manchester City ipo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ikiwa nyuma kwa alama nane dhidi ya klabu ya Arsenal ambao ni vinara wa ligi hiyo, Hivo vijana wa Pep Guardiola watahitaji kushinda mchezo wa leo ili kuendelea kubaki kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza.

