Siku chache nyuma kupitia Meridianbet Sports niliandika kuhusu usajili wa Jean Baleke na Ismael Sawadogo waliosajiliwa na Simba SC kwenye dirisha dogo, huku nikibainisha kuwa Baleke ni moja kati ya straika mwenye uwezo wa ajabu kwenye kufunga. Pata Odds kubwa za soka ukiwa na Meridianbet.

BALEKE

 

Nilienda mbali kiasi kwa mtazamo wangu nikaulinganisha ule mziki wao wakiwa DR Congo kwenye Ligi nchini humo nikasema Utamu wa Congo unahamia Bongo, nilikuwa namaanisha kuhusu Jean Baleke na Fiston Mayele wa Yanga zama zao zinajirudia.

Ikumbukwe kuwa wote hawa walicheza Ligi ya nchini kwao DR Congo na kila mmoja akiwa na timu yake, Fiston Mayele akiwa wa AS Vita na Jean Baleke akiwa na TP Mazembe ya Lubumbashi, moto wao uwanjani ulikuwa ni mkali sana wakichuana kwa kufunga mabao. Beti na Meridianbet mechi za ligi zote, odds ni kubwa sana, Usikose hii!!

 

MAYELE

Mara nyingi Baleke ndiye aliyekuwa akimsumbua sana Mayele, alimnyima kiatu cha dhahabu msimu wa 2020/2021 kwa utofauti wa bao moja tu, 24 kwa 23. Na sasa Jean Baleke moto wake wa TP Mazembe ameuhamishia Bongo pale Simba.

Kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma ilimtosha kwa dakika 46 tu kuamua mechi kwa bao lake la pekee kwenye mchezo huo, huku akifunga kwenye eneo gumu zaidi ambalo linahitaji mshambuliaji mwenye roho ngumu kama yeye. Meridianbet wanatoa ODDS kubwa kwenye mechi zote. Bashiri hapa.

Hivyo kwenye mechi moja aliyocheza akiwa na Simba amefunga bao moja na kiwango chake kilikuwa ni kizuri ttu hivyo kutoa matumaini kwa mashabiki na uongozi wa Mnyama.

Just Imagine Mosses Phiri akipona acheze pale juu na Baleke, Chama arudi , Ntibazonkiza awe kwenye ubora, Sawadogo kwenye dimba la chini akisaidiwa na Kanoute au Mzamiru hiyo Simba itakuaje? Ukiwa na meridianbet unaweza kubashiri mubashara, tembelea maduka ya meridianbet uweze kubashiri.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa