Klabu ya KMC imekubal kichapo cha magoli mawili kwa moja wakiwa katika dimba lao la nyumbani Uwanja wa Uhuru jijini Dar-es-Salaam dhidi ya Dodoma Jiji. Magoli mawili ya Seif Karie yalitosha kuipa ushindi walima zabibu kutoka Dodoma.

Matokeo hayo yanakua sio mazuri kwa klabu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni kwani ni mchezo wapili hawapati matokeo ya kuridhisha baada ya kutoka kupata suluhu mchezo dhidi ya Geita Gold na leo wamepoteza alama tatu dhidi ya Dodoma nyumbani.

Klabu ya KMC Iimeendelea kusalia na alama zake 14 kwenye nafasi ya nane ya msimamo wa NBC huku klabu ya Dodoma jiji ikijisogeza hadi nafasi ya 14 kutoka nafasi ya 15 wakiwa na alama zao 9.

Klabu ya KMC ambayo ilianza ligi vizuri na kushinda michezo kadhaa lakini sasa ni kama ari imepotea na wanadonosha alama kwa uwepesi sana.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa