Uchaguzi Mkuu Simba Mpaka 2023

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa klabu ya Simba, Boniface Lihamwike ameweka wazi kuwa uchaguzi mkuu wa klabu hiyo utafanyika Januari mwaka 2023 na siyo mwaka huu tena kama ambavyo ilitakiwa.

Lihamwike alisema kwa sasa klabu hiyo imeweka malengo kwenye masuala mengine ikiwemo kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kurejesha ubingwa wao wa ligi kuu ambao waliupoteza msimu uliopita.

Akizungumza na kukazia mchakato wa uchaguzi huo kutofanyika kwa mwaka huu, Lihamwike anasema kila kitu kinakwenda kwa mipango Madhubuti kwa uwa yanalenga kuleta mafanikio na tija kwenye timu hiyo.

“Ni kweli muda wa kufanya uchaguzi mkuu umefika kwa mujibu wa katiba ya klabu yetu. Lakini hakutakuwa na uchaguzi kwa mwaka huu kwa kuwa kuna mipango mingine ambayo ni ya msingi pia kwa klabu yetu.

“Uchaguzi utafanyika mwakani mwezi Januari na tutawakuwa tunatoa utaratibu wa uchaguzi huo. Kwa sasa focus yetu ni kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na mashindano ya ndani,” alisema Lihamwike.

Simba walifanya uchaguzi wao Novemba 5, 2018, kuchagua wajumbe wa kamati tendaji na mwenyekiti wa klabu hiyo na kwa mujibu wa katiba yao wanatakiwa kufanya tena uchaguzi huo baada ya miaka minne.

 

Acha ujumbe