KMC Wanyeshwa Wine Uwanja wa Uhuru

Dakika ya 8, 18 Seif Abdallah Kalihe anaiandikia Dodoma Jiji bao la kwanza na la pili. Kwa kichwa akipokea pasi kutoka kwa Paul peter, dakika ya 48 ya mchezo Wazir Jr anasawazisha bao la kwanza kwa KMC.

Klabu ya KMC Kino boys imepoteza mchezo wao dhidi ya mahasimu wao, walima zabibu klabu ya Dodoma Jiji kwa Mabao 2-1, na hivyo kuwafanya kupoteza alama tatu muhimu.

Dodoma Jiji ambao walikuwa ni wageni kwenye mchezo huo, walitangulia kupata mabao yao kwenye kipindi cha kwanza, magoli yakifungwa na mchezaji mmoja Seif Abdallah Kalihe mnamo dakika ya 10 na dakika ya 19, kabla ya Wazir Jr kusawazisha Kino Boys.

Kocha msaidizi wa KMC Hamad Ally mara baada ya mchezo huo alikuwa na haya ya kusema.

“Mchezo haukuwa upande wetu kipindi cha kwanza ndio maana mpinzani wetu akapata magoli mawili, kwa sababu waligundua udhaifu wetu upo upande wa kushoto, na waliutumia na wakafanikiwa”

“Lakini kipindi cha pili tulibadilisha mbinu ya mchezo, tukafanya mabadiliko mawili, (Emmanuel Manu na Majogoro) na mchezo ukabadilika tukapata goli la kusawazisha. Mchezo unaofuata tutafanyia kazi makosa ya leo na kuangalia uwezekano wa kupata alama tatu”

“Kwa upande wa kocha msaidizi wa Dodoma Jiji akizungunza kwa niaba ya Merice Medo alisema kuwa “Waliwatizama vizuri KMC na kugundua udhaifu wao, na kuutumia kupata matokeo kwenye mchezo wa leo”

Tangu kuanza kwa Msimu huu KMC wamekuwa wakipata ushindi kwa tabu, matokeo makubwa yakiwa ni sare.

Acha ujumbe