KMC FC imetamba kuwa imejidandaa vyema kukutana na wapinzani wao Yanga kesho kwenye gemu ya Ligi ya NBC Tanzania.

Klabu hiyo imebainisha kupitia msemaji wake kuwa wamejizatiti kukumbana na mtiti wa Yanga kesho. Kwa mujibu wa msemaji wa klabu hiyo Christina Mwagala, Yanga wana kibarua kigumu sana kwenye mechi ijayo.

KMC, Maandalizi ya KMC Dhidi ya Yanga!, Meridianbet

Katika tambo za msemaji wa klabu ya KMC, amesema kuwa klabu ya Yanga iandae sababu nyingine wasije wakajitetea kuwa Nabi hatakuwepo uwanjani.

“Tumesikia taarifa za kuwa Yanga wameachana na makocha wao wawili, Nabi na Kaze, nasema kabisa mashabiki wao wasije kukigeuza hiki kitu kama sababu ya kujifichia kuhusu kipigo chetu.

“Kwa sababu kwa vyovyote itakavyokuwa lazima tuwafunge, hakuna namna ya wao kukwepa kichapo dhidi yetu. Kwa sababu KMC hii ya sasa haitaki mchezo kabisa na inahitaji alama tatu kwenye kila mchezo.”

Yanga wanatarajia kucheza mechi yao ya saba kwa Mkapa dhidi ya KMC, huku wakiwa wamepishana alama moja tu, Yanga wana pointi 14 na KMC wakiwanazo 13 katika nafasi ya nne na Wananchi wapo nafasi ya pili.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa