Kuelekea mchezo wa kesho jumatano dhidi ya Yanga, Kocha Msaidizi wa KMC, Ahmed Ally amesema kuwa mipango yao ni kupata pointi tatu au ikishindikana waipate moja.

Mchezo huo wa ligi kuu unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo Yanga tayari wakiwa wamekusanya pointi 14 na KMC wakiwa nazo 13.

KMC, KMC Wanazitaka Pointi 3 za Yanga, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi yao, Ahmed amesema wamejiandaa kuelekea kwenye mchezo wa kesho ili kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

“Timu ipo vizuri kuelekea kwenye mchezo wa kesho na mipango yetu ni kuhakikisha tunavuna pointi tatu au ikishindikana tupate pointi moja.

“Tunawaheshimu wapinzani wetu wana kikosi kizuri tumewaona kwenye mechi iliyopita hivyo tumeenda mazoezini na kuandaa mipango mipya kwa ajili ya mchezo huo.

“Makosa ambayo yalifanyika kwenye michezo iliyopita tumeyafanyia kazi na kuyamaliza hivyo hayawezi kujitokeza tena na mashabiki wetu tunawaahidi ushindi.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa