Uongozi wa KMC FC inayodhaminiwa na Meridian Bet umeingilia kati juu ya uwepo wa taarifa kuwa Yanga wameachana na makocha wao wawili, Nasreedin Nabi na msaidizi wake Cedric Kaze kwa kusema kuwa isijekuwa kisingizio cha kipigo chao watachopata kesho kwa Mkapa.

Hayo yalisemwa na msemaji wa timu hiyo Christina Mwagala alipokuwa anazungumzia mchezo wao wa leo wakiwa ugenini dhidi ya Yanga. Tina alisema Yanga wasije wakasema sababu ya kufungwa kwao leo ni sababu ya kukosekana kwa Nabi kwani hata kama wao wangekuwepo kichapo kilikuwa ni halali yao.

KMC, KMC Wafungukia Tetesi za Nabi, Kaze Kufukuzwa, Meridianbet

Christina alisema: “Tumesikia taarifa za kuwa Yanga wameachana na makocha wao wawili, Nabi na Kaze, nasema kabisa mashabiki wao wasije kukigeuza hiki kitu kama sababu ya kujifichia kuhusu kipigo chetu.

“Kwa sababu kwa vyovyote itakavyokuwa lazima tuwafunge, hakuna namna ya wao kukwepa kichapo dhidi yetu. Kwa sababu KMC hii ya sasa haitaki mchezo kabisa na inahitaji alama tatu kwenye kila mchezo.”

Yanga wanatarajia kucheza mechi yao ya saba kwa Mkapa dhidi ya KMC, huku wakiwa wamepishana alama moja tu, Yanga wana pointi 14 na KMC wakiwanazo 13 katika nafasi ya nne na Wananchi wapo nafasi ya pili.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa