Nahodha wa Simba Queens na mshambuliaji kinara wa timu hiyo Opah Clement amesema kuwa wanataka Kwenda kufanya makubwa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Wanawake ikiwemo kuchukua kombe.

Opah alisema anajua kuwa mashindano hayo hayatakuwa rahisi hata kidogo na tageti ya viongozi ni kuipata walau nusu fainali, lakini wao kama wachezaji wanataka Kwenda hadi fainali na kutwaa kombe hilo.

Opah, Opah: Tunalitaka Kombe la Ligi ya Mabingwa, Meridianbet

Opah alisema: “Tumepewa kila kitu na viongozi wetu na ninaweza kusema kuwa Simba Queens ni timu yenye utofauti mkubwa na timu nyingine za wanawake nchini.

“Hiyo ndiyo sababu ya sisi kutaka Kwenda kufanya makubwa huko Morocco. Serengeti Girls wamefika robo fainali kombe la dunia. Sisi tunaitaka nusu fainali na hadi fainali yenyewe.”

Simba wameondoka leo Jumanne na wanatarajia kutua leo jioni nchini Morocco ambacho mashindano hayo yatafanyika na mechi yao ya kwanza watacheza na AS FAR ya Morocco Oktoba 30 na baadae kucheza na Detrmine Girls ya Liberia na kisha Green Buffaloes ya Zambia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa