Mipango ya Hitmana Thiery ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Simba msimu uliopita nyuma ya Mfaransa Didier Gomez, anayeinoa KMC FC amepania kuharibu rekodi ya Yanga yakutofungwa kwenye mechi 43 za ligi kuu.

Mpango huo amepanga kuitimiza kesho kutwa Oktoba 26 uwanja wa Mkapa Dar ambapo watakuwa ugenini kuvaana na Yanga ambayo wikiendi iliyopita walitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na watani zao Simba.

KMC FC, KMC FC Kuchafua Rekodi ya Yanga, Meridianbet

Ofisa Habari wa KMC Christina Mwagala alisema kuwa kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo huo ambao utakuwa ni wa tisa kwao msimu huu Hitmana ambaye ni raia wa Burundi amefanya kila kitu ili kuweza kuimaliza timu hiyo ndani nan je ya uwanja.

“Kocha wetu Hitmana Thiery anajua ugumu uliopo mbele yetu kwenye mchezo huo na Yanga. Lakini ameshafanya kila kitu ili kuvunja rekodi ya Yanga ya kutofungwa kwenye mechi 43 za ligi kuu.

“Tunakwenda kuivunja rekodi hiyo kwa kuwa tuna vijana ambao wanajua nini timu inahitaji. Yanga anakwenda kupasuka na ninasema hivyo kwa kuwa najua mipango yote

“Ninachowaomba mashabiki wa Yanga waje kwa wingi ili walie vizuri na timu yao kwa kuwa pira mapato na pira kodi ndiyo staili ambayo tunakwenda kuwapigia,” alisema.

Yanga na KMC wanapishana alama moja tu, Yanga wapo nafasi ya pili na pointi zao 14, wakati KMC wapo nafasi ya tatu na alama 13, ingawa Yanga wamecheza mechi sita mpaka sasa huku KMC wao wakiwa wameshuka dimbani mara nane.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa