Kocha wa Uganda Amkubali Aziz Ki

Kocha wa Timu ya Taifa ya Uganda, raia wa Serbia Milutin Micho ambaye aliwahi kuinoa Yanga miaka ya nyuma amefunguka kuwa mbali ya kuwa wachezaji wote wa Yanga walicheza vizuri mechi yao dhidi ya Simba ila Azizi Ki alikuwa bora zaidi.

Micho alisema mbali ya lile goli bora la free kick alilofunga Aziz Ki,  pia aliweza kucheza kwa kiwango kikubwa sana kwa dakika zote za mchezo na kwake ndiye aliyekuwa mchezaji bora wa mchezo huo kutokana na kuweza kutimiza majukumu yake vema.

Micho alisema: “Mchezo ulikuwa mzuri sana ila Aziz Ki kwangu ndio alikuwa mchezaji bora wa mchezo , achana na free kick aliyopiga ila nimemfuatilia tangu dakika ya kwanza mpaka mwisho.

“Alikuwa bora sana zaidi ya wachezaji wengine kwenye mchezo ule. Nimependa kila kitu kutoka kwake.”

Mbali na Azizi Ki, Micho alifunguka sababu zilizofanya awepo Dar kushuhudia mchezo akisema kuwa, alikuja kuitazama familia na timu yake ya Yanga na kutazama mechi hiyo kubwa Afrika Mashariki na Kati. Kubwa kumtazama kiungo Kharid Aucho ambaye ni nahodha wa Uganda the crane.

“Licha ya kuja kuangalia moja ya kati ya derby bora kwasasa Afrika mashariki na kati pia jua Yanga ni familia yangu, pia nilikuja kumuangalia moja ya viungo bora kwasasa Khalid Aucho,”

alisema.

Micho aliwahi kuinoa Yanga mwaka 2007 lakini akaja kutimuliwa baada ya timu hiyo kufungwa kwa penalty na Simba  baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ambao ulitumika pia kubadili kalenda ya Ligi Kuu Bara kutoka kuchezwa Januari na Kwenda Agosti.

Acha ujumbe