Uongozi wa Pan African rasmi leo umevunja benchi la ufundi la timu hiyo likiongozwa na Kocha Mkuu, Twaha Beimbaya kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Pan African tangu kuanza kwa msimu huu ikiwa imecheza mechi sita za ligi ya Championship imefanikiwa kukusanya pointi tatu.

Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau imeeleza kuwa “Uongozi unapenda kuwataarifu wanachama, wapenzi na mashabiki kwamba umevunja benchi lake la ufundi kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

“Benchi hilo la ufundi tangu kuanza kwa msimu huu lilikuwa linaongozwa na Kocha Mkuu, Twaha Beimbaya pamoja na Kocha Msaidizi, Hemed Wazir.

“Tunawashukuru sana kwa muda wote ambao wamehudumu katika klabu yetu na tunawatakia kila la kheri katika majukumu yao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa