Pan African Yaipania Pamba

Kikosi cha Pan African kinatarajia kushuka dimbani kesho jumamosi kumenyana na Pamba kwenye mchezo wa ligi ya Championship.

Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza ambapo tayari Pan African imekusanya pointi tatu baada ya kucheza mechi tano.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Pan African, Leen Essau amesema kuwa maandalizi yote kuelekea mchezo huo yamekamilika.

“Wachezaji wana morali kubwa ya kuhakikisha wanapata ushindi wa kwanza tangu kuanza kwa msimu huu kwenye ligi ya Championship.

“Mipango yetu ya kushiriki ligi kuu kwa msimu ujao yapo pale pale kwani tuna kikosi kizuri na benchi la ufundi zuri hivyo tunahitaji kupata pointi tatu za kesho ili kutimiza malengo.”

Acha ujumbe