Kocha Mkuu wa Ihefu, Juma Mwambusi amewalaumu washambuliaji wake kutokana na nafasi walizoshindwa kuzitumia kwenye mchezo wao dhidi ya Singida Big Stars.

Mchezo huo wa ligi kuu ulipigwa jana jumatatu kwenye Uwanja wa Liti, Singida ambapo Singida Big Stars walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Shafiq Batambuzi.

Ihefu, Kocha Ihefu Awalaumu Mastraika, Meridianbet

 

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mwambusi alisema wachezaji wake walitawala mchezo kwa muda wote lakini matokeo hayakuwa upande wao.

“Wapinzani wetu waliitumia nafasi waliyopata ya mpira wa kona wakaitumia kutokana na makosa yaliyofanywa na mabeki wetu.

“Pia upande wa washambuliaji walikuwa na nafasi nzuri ya kusawazisha bao na kufunga la ushindi lakini hawakufanya hivyo kwani muda wote tulikuwa tunamiliki sana mpira.

“Tunaenda kwenye uwanja wa mazoezi kwa ajili ya kufanya marekebisho ya makosa yaliyojitokeza kuelekea mchezo ujao na Azam.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa