Klabu ya Singida Big Stars imepata alama 3 nyingine hii leo kwenye mchezo wao walipokuwa wakikipiga dhidi ya Ihefu ambapo wameshinda kwa bao 1-0, na mchezo huo ulipigwa majira ya saa kumi kamili katika uwanja wa Liti.

 

Singida Big Stars Yapata Alama 3 Dhidi ya Ihefu.

Singida wamepata bao hilo kupitia kwa mchezaji wake Shafik Batambuze katika dakika ya 18 huku ushindi huo ukiwapeleka mpaka nafasi ya 3 baada ya kufikisha pointi 14 wakiwa sawa na Simba na Yanga huku wao wakiwa mbele michezo miwili.

Wakati Ihefu wao wakizidi kuwa na hali mbaya baada ya kupoteza mchezo wa leo wamebaki nafasi ileile ya 14 wakiwa sawa kwa pointi na 5 na Polisi Tanzania pamoja na Dodoma Jiji.

Singida Big Stars Yapata Alama 3 Dhidi ya Ihefu.

Mechi inayofuata ya Singida itakuwa ni dhidi ya Coastal Union ambayo inatarajiwa kupigwa tarehe 30 mwezi huu, wakati kwa upande wa Ihefu yeye atamfuata Azam nyumbani kwake tarehe 31.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa