Kuelekea mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Al MEREIKH Mastaa wa Yanga, Maxi Nzegeli na wenzake wamesema malengo yao kama timu ni kuhakikisha wanapata matokeo mazuri wakiwa ugenini ili mchezo waumalizie hukohuko kabla ya kurudiana Dar.
“Tunahitaji kupata matokeo mazuri tukiwa ugenini ili safari yetu ya kwenda hatua ya makundi iwe rahisi kwa kuwa kama tutashinda ugenini basi hatutakuwa na ugumu sana tukiwa nyumbani.“Tunafahamu ugumu wa mchezo huu, lakini siku zote Ligi ya Mabingwa Afrika haijawahi kuwa na mechi nyepesi kwa kuwa ni mabingwa ambao hukutana,” alisema nyota huyo.
Kwa upande wa Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amesema: “Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ambao utachezwa Rwanda, tunaitaka hatua ya makundi, hivyo mashabiki na Watanzania kwa jumla wazidi kuwa pamoja nasi.”Naye kipa wa Yanga, Metacha Mnata, alisema maandalizi ambayo wameyafanya ni kwa ajili ya kupata matokeo mazuri popote pale iwe ugenini au nyumbani.