Mkude Aagwa Simba Baada ya Muda Mrefu

Kiungo mkongwe  ndani ya klabu ya Simba Jonas Gerald Mkude hatimae amepewa mkono wa kwaheri ndani ya klabu hiyo baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 12.

Jonas Mkude amekua kwenye ubora kwa muda mrefu ndani ya klabu hiyo na akiwa moja ya wachezaji wachache waliodumu ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa lakini hatimae ameweza kupewa mkono wa kwaheri.mkudeKiungo huyo ambaye alianza kuitumkia klabu ya Simba toka kwenye timu ya vijana lakini alifanikiwa kuanza kucheza kwenye timu ya wakubwa mwaka 2011 na ubora wake ulianza kuonekana zaidi katika msimu wa 2012/13.

Jonas Mkude ni mchezaji ambaye anashikilia rekodi ya kucheza mingi ya watani wa jadi ndani ya ligi kuu ya Tanzania kati ya Simba na Yanga mpaka sasa na hii inatokana na yeye kudumu ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu.mkudeKiungo Mkude atakumbukwa zaidi Simba kutokana na utumishi wake uliotukuka ndani ya klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 12, Huku akipata mafanikio makubwa kama kushinda mataji matano ya ligi kuu, FA, na kombe la mapinduzi, bila kusahau kombe la mapinduzi.

Acha ujumbe