Newcastle Yamalizana na Tonali

Klabu ya Newcastle United inaendelea ilipoishia msimu uliomalizika kwani imefanikiwa kumalizana na kiungo wa kimataifa wa Italia anayekipiga katika klabu ya AC milan Sandro Tonali.

Newcastle United baada ya kumaliza katika nafasi nne za juu msimu uliomalizika katika ligi kuu ya Uingereza wameamua kuboresha timu yao kuelekea msimu ujao haswa katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya.NewcastleKlabu hiyo kongwe nchini Uingereza imetoa kiasi cha €milioni 70 kwajili ya kumpata kiungo Sandro Tonali ambaye anafanya vizuri ndani ya kikosi cha Ac Milan katika misimu ya hivi karibuni lakini Magpies wameweza kumng’oa ndani ya viunga vya San Siro.

Newcastle wanapambana sana kuhakikisha wanaiboresha timu hiyo ili iendeleze ubora ambao imekua nao msimu uliomalizika,Hiyo ndio imekua sababu ya klabu hiyo kujitahidi sana kufanya sajili nzuri sokoni kwajili ya kuimarisha kikosi chao.NewcastleKlabu ya Newcastle baada ya kununuliwa na waarabu imekua klabu yenye nguvu na ushawishi sokoni kwani imeweza kusajili wachezaji wenye ubora tena ikishindana na vilabu vikubwa lakini pia klabu hiyo inaweza kupata sajili nzuri nyingi kutokana na kufuzu ligi ya mabingwa ulaya.

Acha ujumbe