Arsenal na Timber Mambo Yanaenda Vizuri

Klabu ya Arsenal ipo kwenye hatua nzuri ya kumalizana na beki wa kimataifa wa Uholanzi anayekipa katika klabu ya Ajax Amsterdam Jurrien Timber.

Arsenal inataarifiwa imeshamalizana na beki huyo kwenye maslahi binafsi na kilichobakia kwa klabu hiyo ni kutuma ofa kwa klabu hiyo, Klabu hiyo inataka kutuma ofa ambayo haitakataliwa wakati huu ili kumalizana na mchezaji huyo moja kwa moja.ArsenalJurrien Timber ameonesha nia ya kutaka kuondoka ndani ya klabu ya Ajax msimu huu na Washika mitutu hao kutoka jiji la London ndio wanaonekana wako mstari wa mbele kumuhitaji beki huyo mwenye ubora mkubwa.

Klabu ya Arsenal inapambana kukijenga kikosi chake kuelekea msimu ujao ambapo inapambana kupata wachezaji wenye uwezo mkubwa sokoni na ndio sababu wanamuwinda beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi.ArsenalArsenal wanamuhitaji sana beki Jurrien Timber kwajili ya kuimarisha kikosi chao haswa kwenye eneo la ulinzi ambalo limeonekana kupitia changamoto wakikosekana baadhi ya wachezaji, Hivo ujio wa Timber utaboresha eneo hilo.

Acha ujumbe