Refaree Alhadi Mahamat Kuamua Mchezo wa Simba Dhidi ya Ahly

Mwamuzi Alhadi Allaou Mahamat mwenye miaka (37) kutoka Chad ndiye atakayeamua mechi ya mkondo wa pili wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba na Al Ahly utakaopigwa leo huko Cairo, Misri.

Refaree Alhadi Mahamat Kuamua Mchezo wa Simba Dhidi ya Ahly

Majira ya saa 5 usiku Simba itashuka katika Uwanja wa Cairo kuamua hatima ya kwenda nusu fainali baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 katika Uwanja wa Mkapa wiki iliyopita.

Mwamuzi huyo aliyewahi kuchezesha mechi ya Yanga ilipopoteza mbele ya CR Belouzdad kwa mabao 3-0 ugenini katika hatua ya makundi, kwenye mechi nane za mwisho alizochezesha mashindano ya kimataifa ametoa mara moja kadi nyekundu.

Refaree Alhadi Mahamat Kuamua Mchezo wa Simba Dhidi ya Ahly
Mahamat alitoa kadi hiyo katika mchezo wa mashindano ya African Football League (AFL) kati ya Enyimba na Wydad AC ambao Enyimba ililala kwa bao 1-0, Oktoba 22, mwaka jana.

Simba inapaswa kucheza kwa uangalifu kwa kuwa ni mwamuzi huyo anapenda kutoa kadi hasa za njano na kwenye michezo nane ametoa 28 ikiwa ni wastani wa kadi tatu kwa kila mchezo.

Pia Alhadi alichezesha mchezo wa ligi ya Mabingwa Barani Afrika kati ya Wydad Casablanca na Simba SC msimu uliopita hatua ya robo fainali na Mnyama kutolewa kwa mikwaju ya penati.

Acha ujumbe