Rekodi Kubwa za Simba Tanzania na Afrika

SIMBA

Tanzania kumekuwa na timu mbili kubwa zenye mashabiki wengi kila kona ya nchi na nje ya nchi, Simba SC ni moja ya timu kubwa Tanzania na Afrika kwa ujumla imekuwa ikifanya mambo makubwa kiasi kwamba tusipoyasema vizazi vyetu vitakuja kutushangaa. Meridianbet Sport tumekuandalia Rekodi za Simba kuanzia mwaka 1936.

 

Simba imepitia majina mengi toka kuanzishwa kwake mpaka sasa. Ilipoanzishwa mwaka 1936 iliitwa Queens jina lilidumu mpaka mwaka 1948 walipofanikiwa kupanda ligi daraja la kwanza na wakati huo mkoa wa Pwani ulianzisha ligi maalumu iliyokuwa ikijiendesha kwa misingi bora ya kisasa.

Wakati huu ndio Simba ilianza kupata ufadhili unaoeleweka mfano jezi nzuri za kisasa na viatu wakati wenzao wakiwa bado wakilisakata kabumbu peku peku . Odds kubwa kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni vitu vinavyoweza kubadilisha maisha yako kwa kukupatia pesa nyingi. Ingia mchezoni hapa.

Simba walibadilishwa jina na kuitwa Eagles baada ya kuonekana jina la Queens linawaletea kebehi kwa watani wao wa jadi Yanga SC ambao kabla ya mwaka 1930 walijulikana ‘ New Young ‘.

Jina la Eagles yaani tai kwa lugha ya kiswahili halikudumu sana. Lilikaa kwa muda mchache sana na kubadilishwa kuwa Sunderland.

Beti na Meridianbet kwa odds kubwa na machaguo kibao, pia unaweza kubashiri mubashara.

Hili ndio jina ambalo wengi wanalifahamu sana . Ni jina ambalo wekundu hawa wa msimbazi wana kumbukumbu nalo kubwa na ndefu kidogo.

Baada ya nchi kupata Uhuru mwaka 1961 na miaka minne baadae kuanzishwa ligi daraja la kwanza yenye sura ya kitaifa yaani ligi iliyoshirikisha timu zote za bara na visiwani, Sunderland ndio ilikuwa timu ya kwanza kubeba kombe la ligi hiyo mwaka 1965 na kulitetea tena kombe hilo mwaka 1966.

Hivyo katika historia Simba SC wakitumia jina la Sunderland waliweza kunyakua ubingwa wa ligi daraja la kwanza mara mbili kabla ya jina hilo kufa mwaka 1971 baada ya raisi wa kwanza wa Zanzibar hayati Abeid Karume kuwashauri kubadili jina kwa sababu ya maudhui yake kikoloni na ndipo jina la Simba SC lilipozaliwa.

Mwaka 1977, Simba iliweka rekodi katika mechi za watani wa jadi kwa kuifunga Yanga mabao 6-0. Zaidi ya miaka 42 rekodi hiyo haijafikiwa.

Mwaka 1938, Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikuwa timu ya kwanza kucheza na jezi ilipocheza na timu ya kombaini ya mabaharia wa meli zinazotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Mwaka 1941, (Sunderland) kwa sasa Simba SC ilikuwa timu ya kwanza nchini kuvaa viatu kwenye mechi rasmi ya mashindano dhidi ya timu ya jeshi la maji la mkoloni la Afrika Mashariki.

Mwaka 1959, kabla ya uhuru wa Tanganyika, kipindi hicho ikiitwa Sunderland (kwa sasa Simba SC) ilikwenda Ethiopia na ikawa timu ya kwanza kutoka nchini kupanda ndege. Ilikwenda kwa mwaliko wa Mfalme Haile Selassie wa Ethiopia.

Mwaka 1965, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania.

Mwaka 1968, Simba ilikuwa timu ya kwanza nchini kumiliki basi lake.

Mwaka 1974, Simba ilikuwa klabu ya kwanza kuwa Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati. Pia mwaka huo Simba ikawa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kufika nusu fainali ya Klabu Bingwa ya Afrika.

Mwaka 1979, Simba ilikuwa klabu ya kwanza na ya pekee duniani kwenye mashindano ya mabara tofauti kufungwa nyumbani magoli 4-0 na kushinda ugenini magoli 5-0 (dhidi ya Mufulira Wanderers).

Mwaka 1993, Simba ilikuwa klabu pekee nchini kuwahi kufika fainali ya mashindano yanayoandaliwa na CAF (kwa sasa Kombe la Shirikisho) na kucheza fainali na klabu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast.

Simba ndio mabingwa wa muda wote wa Kombe la Afrika Mashariki na Kati (makombe 6).

Mwaka 2003, Simba ilivunja rekodi ya Zamalek ya Misri kwa kuitoa kwenye Ligi Mabingwa Afrika na kutinga hatua ya makundi. Zamalek walikuwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo.

Mei 6 Mwaka 2012 simba iliinyuka Yanga mabao matano kwa nunge kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa wafungaji wakiwa ni Felix Sunzu akifunga mara mbili Emanuel Okwi akifunga mara moja marehemu Patric vierra Mutesa Mafisango pamoja na Juma K Juma ..

Simba ndio klabu yenye makombe mengi ya jumla kuliko klabu yoyote Afrika Mashariki, ikiwa na vikombe rasmi vya kimashindano hamsini na nane(58).

Tembelea duka la ubashiri-Meridianbet kutandika jamvi lako kwa odds kubwa.

Acha ujumbe