Klabu ya Simba inaongoza goli moja hadi sasa dhidi ya KMC kipindi cha mapumziko (45) ambapo bao hilo limefungwa na mshambuliaji John Bocco katika dakika ya 15 ya mchezo.

Simba wanafanya mashambulizi mengi sana kwenye lango la KMC wakihitaji kupata bao lingine ili waweze kujihakikishia pointi 3 kwani bao moja halitoshi kuwafanya wao kuwa salama.
KMC licha ya kuwa wametanguliwa wanajitahidi kufika langoni kwa mpinzani lakini walinzi wa Mnyama wamekaa imara kuhakikisha kuwa lango lao halitikiswi huku golikipa Manula akifanya jitihada kuokoa mipira yote inayokuja.

Timu zitaraejea kumalizia dakika 45 zingine ambapo vijana wa Thierry Hitimana wanaweza kufanya mabadiliko au kwa Wekundu wa Msimbazi nao wanaweza kuingiza baadhi ya wachezaji ili kuongeza nguvu.

