UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa usajili ambao wameufanya msimu huu unastahili kwao kufanya vyema msimu ujao haswa kuyarudisha mataji yote ambayo wameyapoteza kwa misimu kadhaa.

Simba mmpaka sasa wamefanya usajili wa wachezaji wa maana wa kimataifa kama Luis Miquissone, Aubin Kramo, Essomba Onana, Fabrice Ngoma na kipa kutoka Brazil, Jefferson Luis.simbaMeneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmedy Ally alisema kuwa kwa majembe ambayo wamayashusha yakiongozwa na Luis Miquissone ni wazi kuwa matarajio yao ni kuhakikisha kuwa wanabeba mataji yote msimu ujao ambayo waliyapoteza kwa kuwa watakuwa na kikosi bora.

“Huu usajili ambao tumeufanya ni balaa tupu kwani majembe ambayo tumeyashusha ni wazi kuwa msimu ujao kazi yetu itakuwa kuhakikisha kuwa tunayarudisha mataji yetu yote ya ndani ambayo tuliyapoteza misimu miwili iliyopita.simba“Wapinzani wetu wajiandae kwani safari hii tumeshusha vyuma ambavyo vinaakisi nini tunahitaji msimu ujao katika kila mashindano ambayo tutashiriki, kuanzia mashindano ya ndani mpaka yale ya nje,” alisema kiongozi huyo.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa