Simba Imekamilika, Fadlu Davids Aanza Kazi Rasmi

SIMBA WANA HASIRA NYIE, Ni kipigo cha Bao 7-2 kutoka kwa watani zao Yanga? ni kukosa ubingwa kwa misimu mitatu? au Tajiri MO Dewji kuambiwa hana pesa? MAANA vyuma hivi vilivyotua Msimbazi wapinzania watafute pakujificha. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Simba hakuna sehemu ambayo haijafanyiwa maboresho yeyote yale, upande wa benchi la ufundi, Viongozi, Kamati za Utendaji, Wachezaji wa kila eneo kuanzia mabeki, viungo na wshambuliaji.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

BENCHI LA UFUNDI

Simba dilisha hili limefanya mapinduzi kwenye eneo la benchi la ufundi kwa kumbakiza Seleman Matola pekee huku wakishusha makocha wanne kwenye maeneo mbalimbali. Matola ndiye kocha mwenye umri mkubwa pia kulinganisha na wenzake waliopo kwa sasa, akiwa na miaka 46.

Kocha mkuu, Fadlu Davids ana umri wa miaka 43 tu na amefanya kazi na makocha wengi wenye uzoefu mkubwa akiwa Raja Casablanca. .

Kocha huyo anachukua nafasi ya Benchikha aliyeondoka mwishoni mwa msimu na kuiacha timu mikononi kwa Juma Mgunda aliyemaliza mkataba Msimbazi.

Fadlu ametua na wasaidizi wanne akiwamo Darian Wilken (29), Wayne Sandilands (40) anayenoa makipa, kuna mtathmini wa video, Mueez Kajee anayetajwa kuwa na umri usiofika miaka 38 na kocha wa viungo, Riedoh Berdien (42).

Makocha hao wapya wakiungana na Matola wanachukua nafasi zilizoachwa wazi na Benchikha aliyeondoka na wasaidizi wawili, Kamal Boujnane na Farid Zemit, sambamba na Dani Cadena aliyekuwa akiwanoa makipa na Culvin Mavunga aliyekuwa mtathmini wa video kutokea Zimbabwe.

MAKIPA

Eneo hili Simba haijafanya usajili ni wazi kuwa wataendelea na makipa wao wa msimu uliopita ambao ni Ayoub Lakred, Aishi Manula ambaye anatajwa kutua Azam FC kwa mkopo, Ally Salim, Ahmed Feruzi na Hussein Abel.

Kati ya makipa hao watano Lakred ndiye kipa namba moja baada ya Manula kutupwa benchi tangu alipopata jeraha la nyonga akikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

MABEKI

Eneo hili Simba limefanya maboresho kwa kuongeza wachezaji wapya kila hadi beki namba mbili ambayo tayari ina Shomari Kapombe, David Kameta ‘Duchu’ na Israel Mwenda ambao wataendelea kubaki ndani ya timu hiyo.

Simba pia imemsajili Kelvin Kijiri anayeenda kusimama eneo hilo kutokana na taarifa kwamba Mwenda amesaini pia Singida Black Stars.

Eneo la beki namba tatu ambalo lilikuwa bora chini ya nahodha msaidizi Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye anarekodi nzuri kwa kucheza misimu minne mfululizo kwa ubora ule ule ameongezewa nguvu baada ya kufanya usajili wa Valentin Nouma (24) akitokea timu ya St. Eloi Lupopo ya DR Congo.

Beki ya kati ambayo ilikuwa bora chini ya Henock Inonga na Che Malone Fondoh imeongezwa nguvu baada ya kufanya biashara ya Inonga kwenda FAR Rabat ya Morocco na kuwamsajili Chamou Karaboue ili kuziba pengo hilo.

Simba pia imemsajili mzawa Abdulrazack Mohamed Hamza (23) akitokea Supersport United ya Sauzi samba na kuwepo kwa Hussein Kazi ambaye hata hivyo inaelezwa huenda akapelekwa kwa mkopo Singida Black Stars dili ambalo bado halijakamilika.

KIUNGO

Eneo hili Simba haijataka kufanya masihala mara baada ya kuondoka kwa Said Ntibazonkiza ‘Saido’, Luis Miquissone, Sadio Kanoute na Clatous Chama ambao mikataba yao iliisha, imefanya usajili wa wachezaji wa watano, wanne wa kigeni na mmoja mzawa ambao tayari hadi sasa imewatambulisha.

Ilianza na Joshua Mutale (22), Augustine Okajepha (20), Debora Mavambo (24), Jean Charles Ahoua (22) na Yusuf Kagoma (28) ambao wote wanacheza eneo la kiungo hivyo ni wazi wamejipanga kutengeneza timu kwenye maeneo yote, mbali na ongezeko hilo pia Simba bado ina Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma ambao wataendelea kubaki ndani ya kikosi hicho baada ya kufanya vizuri msimu ulioisha.

Kuna wazawa wawili wapya pia walioongezwa katika eneo hilo akiwamo Awesu Awesu aliyekuwa KMC na Omary Omary kutoka Mashujaa, hivyo kulifanya eneo hilo la kiungo kuwa na vichwa vya kutosha kwa sasa.

STRAIKA

Eneo la ushambuliaji ambalo limekuwa likifanyiwa maboresho mara kwa mara baada ya kuondoka kwa Moses Phiri na Jean Baleke, Simba imefanya usajili wa mchezaji mmoja tu ambaye ni Steven Mukwala ambaye ametoka Asante Kotoko ya Ghana.

Mshambuliaji huyo msimu ulioisha akiwa Kotoko ameifungia timu yake mabao 14 na kutoa pasi mbili zilizozaa mabao kwenye mechi 28 za ligi, anaungana na Kibu Denis eneo hilo ambaye ameongeza mkataba wa miaka miwili pamoja na Freddy Michael ambaye amesalia kikosini baada ya kutua katika dirisha dogo lililopita.

Katika nusu msimu alioitumikia Simba, Freddy amefunga mabao sita katika Ligi Kuu Bara na mengine ya Kombe la Mapinduzi, Kombe la Shirikisho la michuano ya CAF. Pia kuna ingizo jipya la Valentino Mashaka (18) kutoka Geita Gold.

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

Acha ujumbe