Wekundu wa Msimbazi- Simba SC wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa mashindano ya Kombe la Mapinduzi huko kwenye visiwa vya marashi na karafuu- Zanzibar na hivyo kufanya kuvuliwa ubingwa wao aliouchukua mwaka jana 2021/2022.

Mnyama alicheza jana usiku dhidi ya Mlandege na kupoteza kwa bao 1-0 bao lililofungwa dakika ya 74 na mchezaji Abubakar Mwadin lilitosha kuvua taji la Simba SC kama bingwa mtetezi na hatimaye kumuondosha kwenye mashindano hayo.
Inakuaje Simba atoke na Ikiwa kacheza mechi moja?
Iko hivi ni wengi wanajiuliza Simba aliyecheza mechi moja tu inakuaje ametolewa kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi, ni kwa sababu kundi C alilopo Mnyama lina timu tatu tu Mlandenge, KVZ FC na Mnyama mwenyewe.
Katika mchezo wa kwanza wa Kundi C, Mlandenge alitoa sare na KVZ FC na jana Mlandege ameshinda hivyo anakuwa na alama 4, Mchezo wa mwisho Mnyama atacheza na KVZ ikitokea Mnyama akashinda hata goli 5 anakuwa na alama 3 ambazo zinamfanya awe nafasi ya pili nyuma ya Mlandege mwenye alama 4.

Hivyo kulingana na kundi lilivyo mechi ni mbili tu na sio tatu, na kwenye kundi hilo ni timu moja tu ndiyo inafuzu kuingia hatuna ya nusu fainali na mpaka sasa Mlandege tayari amajikatia tiketi ya kufuzu hatua ya nusu fainali, hivyo mchezo unaofuata ni wa kukamilisha ratiba tu.

