SIMBA WAWAACHA MBALI WATANI ZAO

SIMBA mapema tu ilikamilisha lengo la kuandika rekodi mpya ikiwapoteza watani zao wa jadi Yanga katika tamasha lao.

Simba ilikuwa ni Agosti 6 2023 iliandika rekodi hiyo kwenye tamasha la Simba Day ikiwa ni tamasha lililokusanya mashabiki wengi nje na ndani ya uwanja.simbaKutokana na jambo hilo Simba inayonolewa na Kocha Muu, Roberto Oliveira ilikamilisha mpango wa kuandika rekodi mpya baada ya majira ya saa mbili asubuhi mashabiki kuanza kuingia uwanjani tayari kwa kushuhudia sherehe za Simba Day.

Hapo awali uongozi wa Simba ulitangaza kufungua mageti saa mbili asubuhi jambo ambalo liliwafanya mashabiki wa timu hiyo kufika mapema na kuanza kuingia uwanjani.

Mashabiki wengi waliotupia uzi wenye rangi nyeupe na nyekundu walikuwa uwanjani kushuhudia namna shughuli hiyo itakavyokuwa.
Lakini hiyo haitoshi rekodi nyingine ni ile ya mashabiki wa Simba hadi kufikia saa 5 asubuhi kujaza nusu ya uwanja wakisubiri shughuli yao ya Simba Day.simbaMwisho kabisa mpaka tamasha linakamilika uwanja ulikusanya full haouse kutokana na hamasa kubwa iliyofanyika kila kona.

Mchezo uliokuwa unasubirwa kwa shauku kubwa ni ule wa kimataifa wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Power Dynamo na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-0 Power Dynamo.

Acha ujumbe