Klabu ya Simba, baada ya kufunga mwaka kibingwa kwa kuichabanga Tanzania Prisons mabao 7-1 yaelekea Zanzibar kwaajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo watakipiga dhidi ya Mlandege.

Simba na Mlandege mchezo wao utapigwa majira ya saa 2:15 baada ya mchezo wa Azam kumalizika huku timu hiyo ya Juma Mgunda akitazamia kuchukua taji hilo tena msimu huu.
Wekundu wa Msimbazi ndio mabingwa watetezi wa Kombe hili walipomtoa Azam FC kwenye mechi yao ya Fainali huku kukiwa na malalmiko kwa baadhi ya viongozi na wachezaji wa klabu ya wanalamba lamba baada ya kupoteza.

Mnyama yupo nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi baada ya kujikusanyia alama 44 kwenye michezo 19 ambayo amekwishacheza hadi sasa. Atarejea kwenye ligi kukiwasha dhidi ya Mbeya City mwezi wa pili.

