JOHN Bocco nahodha wa Simba ameweka wazi kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kupata matokeo ya ushindi kwenye mechi zote wanazocheza ikiwemo ya leo dhidi ya Prisons.
Mchezo unafuata wa Simba ni dhidi ya Tanzania Prisons unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Mkapa saa 12:15 jioni.

Ni mchezo wa kisasi kwa Prisons kwani mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Sokoine Mbeya ulisoma Tanzania Prisons 0-1 ambapo bao la ushindi lilifungwa na Jonas Mkude.

Mkude alitumia pasi ya mwamba Kibu Dennis ambaye alitoa pasi yake ya kwanza msimu wa 2022/23.
Bocco amesema:”Tunajua ushindani kwenye ligi ni mkubwa nasi tunahitaji kupata matokeo chanya kwenye kila mechi,”.

