Klabu ya Simba imeendelea na mazoezi yao kabla ya kusafiri kuelekea Tanga kwenye mchezo wao wa Ligi kuu ambao wanarajia kucheza dhidi ya Coastal Union ya mkoani Tanga hapo keshokutwa.

 

Simba Yaendelea na Mazoezi Kabla ya Kuifuata Coastal union

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi huku wakiwa wameshinda mechi zake tisa, wakiwa wametoa sare nne na kupoteza mechi moja wakiwa wamejivunia pointi 31 hadi sasa.

Wakati kwa upande wa Coastal Union wao wapo nafasi ya 12 wakiwa wamepata ushindi mara tatu, sare tatu na kupoteza mechi saba wakijikusanyia pointi zao 12 ambazo hazitoshi kuwaweka salama hadi sasa.

Coastal Union wametoka kupoteza michezo minne mfululizo huku mechi ya Azam ambayo walicheza Chamazi wakidondosha alama zote kwa uzembe wa kupoteza muda na baadae kumshambulia mwamuzi kutokana na uzembe wao.

 

Simba Yaendelea na Mazoezi Kabla ya Kuifuata Coastal union

Simba wao wametoka kupata ushindi mnono dhidi ya Polisi Tanzania huku mshambuliaji wao ambaye anaongoza mabao kwa upande wa vijana wa Jumma Mgunda Mosses Phiri akitupia mawili kambani.

Mechi iliyopita kukutana timu hizi mbili, Coastal alipoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Simba wakiwa nyumbani kwao, huku Jumamosi wakitafakari njia ya kuzipata alama tatu wakae nafasi nzuri.

Simba Yaendelea na Mazoezi Kabla ya Kuifuata Coastal union


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

BONYEZA HAPA KUCHEZA

 

 

Simba, Simba Yaendelea na Mazoezi Kabla ya Kuifuata Coastal union, Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa