Klabu ya Simba leo imeingia mkataba na Kampuni ya Bima ya MO Assuarance wa kuigharamia katika masuala ya Afya na matibabu ya wachezaji wa Simba, Simba Queens, Benchi la Ufundi, wafanyakazi wote wa klabu hiyo na Familia zao.
Kupitia C.E.O wao Barbara Gonzalenz amesema kuwa; “Leo tunaingia rasmi kwenye ushirikiano na Mo Assurance kama mshirika rasmi wa bima wa Simba SC”.
Lakini pia aliongezea kwa kusema ushirikiano huo ni mzuri kwani utawawezesha wachezaji pamoja na familia zao kupata huduma hiyo kwa haraka zaidi.
Mkataba huo ni wa miaka miwili wa bima ya afya kwa wachezaji, benchi la ufundi na menejimenti ya Wekundu wa Msimbazi na kampuni ya Bima ya MO Assuarance kwa kipindi cha miaka miwili wenye thamani ya Tsh. 250 milioni.
Mkurugenzi mtendaji wa MO Assuatance Gregory Fortes, amesema kuwa wao kama kampuni wameamua kutoa bima ya afya, huku kukiwa na aina tofauti kama watu wanaolazwa, wanaokwenda kutibiwa na kurudi nyumbani kwao na mambo mengine madogodogo kama matatizo ya meno, macho lakini pia wameongeza huduma ya majeraha yanayotokana na michezo.