Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Marcus Rashford amebakiza goli moja ili kufikisha magoli 100 ndani ya klabu ya klabu hiyo. Na hiyo ni baada ya kufunga goli katika mchezo wa jana dhidi ya Sheriff katika mchezo wa Uefa Europa ligi.rashfordManchester United jana walifanikiwa kupata ushindi wa magoli matatu kwa bila dhidi ya klabu ya Sheriff katika mchezo wa tano wa kundi C katika michuano ya Uefa Europa League iliopigwa katika dimba la Old Trafford.

Mshambuliaji Rashford aliweza kufunga bao la pili la mchezo na kuweza kufikisha goli lake la 99 tangu aanze kuitumikia klabu hiyo tangu alipopandishwa kwenye timu ya wakubwa mwaka 2015 chini ya kocha Louis Van Gaal.

Mshambuliaji huyo wa kiingereza amekua kwenye kiwango kizuri msimu tofauti na msimu uliomalizika lakini mpaka sasa msimu huu ameonesha kiwango kikubwa chini ya mwalimu Eric Ten Haag.rashfordMarcus Rashford mpaka sasa amefunga magoli sita huku akipiga pasi za mwisho za mabao tatu mpaka huku akiipita rekodi yake akiwa amefunga magoli matano kwa msimu msima. Hivo hii inaonesha kwa namna gani ameboresha kiwango chake kwa kiwango kikubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa