Marcus Rashford mchezaji wa klabu ya Manchester United amefanikiwa kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa tisa kunako ligi kuu ya uingereza.

marcus RashfordTuzo hizo ambazo husimamiwa na kampuni ya kielektroniki inayohusika na kuzalisha maudhui ya kimichezo ya EA Sports imemtangaza mchezaji huyo wa klabu ya Manchester United kua mchezaji bora wa mwezi huo baada ya kua na kiwango bora kabisa ndani ya mwezi huo.

Marcus Rashford amekua na kiwango bora ndani ya mwezi wa tisa baada ya kuonesha uwezo wa hali ya juu katika michezo miwili aliyocheza ndani ya mwezi huo na kuhusika na magoli manne.

Mchezaji huyo amefunga magoli mawili na kutoa pasi mbili za mabao katika michezo miwili aliyocheza ambayo ni dhidi ya Leicester ambapo alipiga pasi ya bao huku mchezo dhidi ya Arsenal ambapo alipiga pasi moja ya bao na kufunga mabao mawili.

marcus rashfordMarcus Rashford ameanza vizuri msimu huu baaada ya kua msimu mbaya mwaka 2021/22 lakini anaonekana anaanza kurudisha makali yake katika msimu huu ambapo mpaka sasa ameshafunga mabao matatu na kupiga pasi mbili za mabao jambo ambalo halikua rahisi kwa msimu uliomalizika.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa